Home Kimataifa Vigogo wa Rwanda waliomhonga refa watiwa mbaroni

Vigogo wa Rwanda waliomhonga refa watiwa mbaroni

9081
0

Mabosi wa chama cha soka cha Rwanda FERWAFA waliokumbwa na kashfa ya kuhonga refa kwa sasa wanatumia ndoo za korokoni.


Tumezoea kusikia kuwa marefa wamehongwa lakini hatujawahi kusikia wanaowahonga ni akina nani. Kule Rwanda hali imekuwa tofauti kidogo. Mwamuzi aliyehongwa atoboa siri.

Ferwafa ipo kwenye moshi wa matakataka na hatujui kama viongozi wake watatoka salama, Francois Regis Uwayezu kulia pichani na kamishna wa mashindano Eric Ruhamiriza kushoto pichani wamewekwa kwenye kiti cha moto baada ya kukumbwa na kashfa ya kuhonga waamuzi.

Kwani mchongo mzima upoje?

Hawa viongozi wa Rwanda walimhonga mwamuzi kutoka Namibia ambaye alichezesha mchezo wa Rwanda dhidi ya Ivory Coast.

Serikali ya nchi hiyo imechukua uamuzi gani?

Modeste Mbabazi, msemaji mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa makosa nchini humo (Rwanda Investigations Bureau (RIB)) amesema viongozi hao wa chama hicho walishikwa mara moja baada ya tuhuma hizo.

Huyo Refa, khaa.. Kuna marefa wengine kweli ni mashujaa. Kibongo bongo kweli inawezekana hii?

Kwanza ilikuwaje kwani?

Huyo refa anajulikana kama Jackson Pavaza, na alipangwa kuchezesha mchezo huo ndani ya uwanja wa Nyamirambo. Kabla ya hapo Pavaza alitoa malalamiko yake mbele ya waandishi wa habari akidai kuwa kuna watu wamekuwa wakimsumbua wakitaka wampe rushwa.

Halafu ikawaje?

Inaonekana baada ya sekeseke zima serikali ya Rwanda ikaamua kujitosa yenyewe baharini kabla mkono FIFA haujatembeza rungu lao.

“Watuhumiwa wote tushawaweka rumande, vigogo hawa walituhumiwa kwa kumhonga mwamuzi ambaye alikuwa anapaswa kuchezesha mchezo wa timu yetu ya taifa  (Amavubi) na Les Eléphants ya Côte d’Ivoire, na uchunguzi wetu bado unaendelea,” Alisema Mbabazi.


Nilitamani sana kujua kiasi gani walijaribu kumhonga? Na walimhonga vipi?

“Kwa sasa hatuwezi kusema chochote kuhusiana na taarifa hizo. Hizo ni taarifa za ndani sana na uchunguzi bado unaendelea” Mbabazi

Washukiwa wapo wapi sasa?

Washukiwa wote kwa sasa wapo kituo cha polisi cha  Kimihurura.


Hata hivyo mchezo huo ulikwenda kwa Rwanda kupata kichapo cha 2-1.

Viongozi hao wa FERWAFA nao wana lipi?

Wamesema hayo mambo hawayajui. Ni lengo la kiwachafua hawafaham lolote.

Wadau wanasema vipi?

“Marefa wetu wajifunze. Haya mambo hayaanzii ukubwani. Lazma ujizoeshe kuanzia mechi za mchangani” alisema Issa Masoud CPA mhasibu mkuu wa clouds media Group 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here