Home Ligi EPL Wachezaji wa kigeni wanavyozidi kuiua La Masia katika ramani ya soka la...

Wachezaji wa kigeni wanavyozidi kuiua La Masia katika ramani ya soka la Hispania

12112
0

Kwa siku za hivi karibuni Real Madrid imeipiga bao Barcelona kwa kutoa idadi ya wachezaji wengi wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Hispania. Kuna mabadiliko, siku za nyuma wakati Hispania wanashinda Euro na kombe la dunia wachezaji wa Barcelona ndio walikuwa uti wa mgongo wa timu ya taifa ya Hispania.

Wachezaji hao walikuwa wametengenezwa kwenye academy yao ya La Masia akina Xavi, Puyol, Valdes (golikipa namba mbili nyuma ya Iker Casillas), Pedro, Iniesta, Busquest, Fabregas.


Kwa sasa kumetokea mabadiliko, wachezaji hao wakati wao umefika kikomo wameondoka. Sasa hivi Barcelona inaundwa na wachezaji wengi wa kigeni, Golikipa Mjerumani Ter Stegen, Umtiti-Ufaransa, Rakitic-Croatia, Coutinho-Brazil, Dembele-Ufaransa, Suarez-Uruguay, Messi-Argentina, achana na wazawa akina Pique ambaye amestaau timu ya taifa.


Hiyo ndio Barcelona ya sasa hivi ambapo wachezaji wakiitwa timu ya taifa labda Sergio Roberto, Jordi Alba wanaweza kuitwa (lakini tayari Alba hana uhusiano mzuri na kocha Luis Enrique) ndio maana hajamwita kwenye kikosi chake, kwa hiyo Barcelona inavyoendeshwa sasa hivi ndio inapelekea uwakilishi mdogo kwenye timu ya taifa.


Turudi upande wa pili ambapo Real Madrid yenyewe imejaza wahispaniola kwenye kikosi chake. Kikosi cha Hispania kilichoanza jana dhidi ya Croatia kilikuwa na wachezaji sita (6) wa Real Madrid Carvajal, Ramos, Nacho, Isco, Asensio, Ceballos.


Kwa hiyo timu ya taifa inapochaguliwa wanaangalia wachezaji ambao wanacheza na wana-perform kwa wakati huo, kwa sasa Madrid inajengwa na wazawa wengi.

Hoja inayojitokeza hapa ni kwamba, wakati timu ya taifa ya Hispania inabebwa na Barcelona mafanikio waliyoyapata yalikuwa ni makubwa pia wanajivunia kuchukua Euro na kombe la dunia, je katika zama hizi Hispania itafikia mafanikio yaliyofikiwa wakati inabebwa na Barca?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here