Home Kimataifa Wakala wa Pogba, Mino Raiola atibuana na Scholes

Wakala wa Pogba, Mino Raiola atibuana na Scholes

10183
0

Kama kuna mawakala wahuni chini ya hili jua kwenye masuala ya soka basi Raiola ni namba moja. Jamaa anajua sana kucheza na akili za watu. Yaani ni mtoto wa mjini. Kila nikimuona nakumbuka sakata lake la kurushiana vijembe na Zlatan lakini baadae akaja kuwa wakala wake.

Anajua kucheza na vyombo vya habari. Tofauti yake na Mendez, Mendez yeye ni mtu wa mambo smati. Hana kelele nyingi na mambo yake yanaenda kisomi. Ni tofauti na Mino. Mino anaweza kumchochea mchezaji ili tu aondoke. Mino ana migogoro na vilabu vingi tu kama Ac Milan na hata Juventus.

Tumesikia hivi majuzi Pogba anataka kuondoka. Mbaya zaidi Paul Scholes amemjia juu Pogba hasa kwa kiwango chake.

Kuna kila Ishara kuwa Mino anataka Pogba aondoke Man united. Kocha mkuu wa Zamani wa Man United aliwahi kusema kati ya wakala 1 au hata wawili ninaowachukia basi Mino Raiola ni mmoja wao. Ferguson alikiri kuwa Paul Pogba akikuwa kijana mzuri lakini shida alikuwa na wakala mwenye chokochoko nyingi sana. Raiola alikuwa akifukunyua taratibu za usajili za Manchester kihuni huni tu ili kujua madhaifu na maswahibu ya klabu.

Tumeona kwenye mtandao wake wa Twitter amemtumia Scholes ujumbe.

“Kuna watu wanaongea sana kwa kuwa wanaogopa kusahaulika. Paul Scholes asingetambua kama mbele yake kuna kiongozi hatakama angekuwepo mbele ya Sir Winston Churchill. @paulpogba”

Ujumbe huu unashiria kuwa Scholes anaongea sana kwenye vyombo vya habari ili mashabiki wa Man United wasimsahau. Mino anaamini kuwa Scholes haoni ubora wa Pogba ndio maana kila uchao anamuongelea vibaya.

Lakini mashabiki wa Man United pia wamemjia juu na kumwambia Scholes alisimama mbele ya Roy Kean ambaye alikuwa kiongozi hivyo Scholes ana upeo mkubwa wa kutambua nafasi za watu.

Mino akaweka tena ujumbe mwingine

“Paul Scholes anapaswa kuwa mkurugenzi wa michezo ili amshauri Woodward kumuuza Pogba. Nitapoteza usingizi wangu usiku kucha na kuhakikisha Pogba anapata klabu mpya @paulpogba

Inaashiria kuwa Mino anawachokoza Man United, anamtoa Pogba mchezoni na anahakikisha kuwa mambo hayaendi sawa. Ni wazi Pogba ni mchezaji mzuri sana. Matumizi yake uwanjani yanamnyima amani. Kocha mkuu wa Ufaransa pia aliwahi kukiri kuwa Pogba hana amani United. Anashindwa kuliweka wazi hilo kwa kuwa rohoni anaipenda United kuliko mfumo wa Mourinho.

Tumeona mchezo wa juzi dhidi ya Brighton Pogba amepoteza takribani mipira 27. Ingetokea siku Scholes akapoteza mipira mingi hivyo basi siku hiyo hiyo angetangaza kustaafu.

Mafanikio ya Paul Scholes Manchester United:

πŸ”΄ Michezo: 718
⚽️ Magoli: 155
πŸ† Makombe ya ligi kuu: 11
πŸ† FA Cups: 3
πŸ† Vikombe vya ligi: 2
πŸ† Champions League: 2
πŸ† Ngao ya Hisani: 5
πŸ† Club World Cup: 1

Hebu tuone filamu hii mwisho wake utakuwa wapi.. Niwakumbushe tu, wakati Mino anamleta Pogba Man United mara ya pili watu wakamwita supa agenti sijui akimuondoa Pogba watamuitaje…

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here