Home Ligi EPL Wakati saga lake na Pogba bado la moto, De Bruyne amchana Mourinho

Wakati saga lake na Pogba bado la moto, De Bruyne amchana Mourinho

17784
0

Mambo ni motoo Old Traford, mvutano kati ya Jose Mourinho na kiungo Paul Pogba ni wa moto huku kila mmoja akiongea yake lakini sasa ni wazi kwamba mafahali hao wawili hawakai zizi moja.

Wakati Jose na Pogba wakiendelea kuvutana, Kelvin De Bruyne ameibuka na kusema maamuzi ya kocha Jose Mourinho ndio ambayo yalimfanya kuitosa Chelsea mwaka 2014.

De Bruyne anasema alikuwa mtoto mdogo na alikuwa akitaka muda wa kucheza soka lakini baada ya muda Mourinho aliacha kumpa nafasi uwanjani na hii ikamfanya amtose.

“Nilikuwa kijana mdogo tu wakati najiunga na Chelsea (20), wakati najiunga nao nilikuwa ninapewa nafasi lakini baadaye mambo yalibadilika, nilihitaji kucheza hivyo nikaamua kuondoka”

Mourinho alimuanzisha De Bruyne katika michezo miwili tu EPL na mwingine akamuanzisha kama sub huku Champions League michezo yote mitatu aliyoingia aliingia kama Sub.

Wakati Mourinho anamuacha De Bruyne alimchana wazi mbele ya vyombo vya habari kwa kusema kwamba alikuwa hapendu namna De Bruyne anavyocheza mazoezini na hata baadhi ya mechi ndio maana akamtosa.

Wakati Mou alimponda De Bruyne ,upande wa pili kocha wa Man City amesema De Bruyne ni mchezaji mkali sana ila ana aibu mazoezini na huwa haongei ndio maana unaweza usimuelewe kwa haraka.

Kwa sasa De Bruyne ni majeruhi, na majeraha yatamuweka nje miezi miwili huku msimu uliopita alikuwa nguzo kubwa kwa Man City kubeba ubingwa wa EPL.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here