Home Ligi EPL Wakati wakiendelea kuwaza beki wa kati, tatizo jipya laibuka Manchester United

Wakati wakiendelea kuwaza beki wa kati, tatizo jipya laibuka Manchester United

10898
0

Kati ya maeneo ambayo sio tu mashabiki wa Manchester United bali hata kocha Jose Mourinho hana imani nayo United baasi ni beki wa kati ambaye atakuwa anacheza na Eric Bailly.

Hii ndio sababu kubwa katika usajili ulikuwa unaona United wanahusishwa na kununua mabeki wa kati tu kama Jerome Boateng, Godin na wengine kama Harry Maguire.

Mourinho hamuamini Rojo, Mourinho hamuamini Smalling wala Jones na baada ya kupata kiungo (Fred) alitamani kukamilisha usajili wa beki mmoja mkubwa akiamini ndio angemaliza matatizo United.

Lakini katika mechi ya kwanza tu kati ya Manchester United vs Leicester City United wameonekana na tatizo jingine ambalo linaonekana kubwa zaidi kuliko la beki wa kati, UPANDE WA KULIA.

Ukiangalia mchezo kati ya Leicester City vs United unaweza kushangaa namna Mata na Darmian walivyokuwa wakicheza na kubaki kujiuliza hivi hawa nini kimewakuta hadi eako hivi?

Pengine labda ni kwa sababu Valencia hayupo kwani Leicester City walikuwa wakiisababishia sana United eneo la kulia na Denarai Gray kuonekana kama Messi kutokana alivyokuwa akiwakimbiza kulia.

Lakini yote tisa, ila kumi Jose Mourinho mwenyewe anaonekana ameshakata tamaa kwa msimu huu kwani anaamini klabu haijasikiliza mipango yake ya usajili na hii inawafanya kuwa na wakati mgumu zaidi msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here