Home Uncategorized Wakiwa hawajayasahu ya Tottenham, Sadio Mane arusha kombora Manchester United

Wakiwa hawajayasahu ya Tottenham, Sadio Mane arusha kombora Manchester United

14613
0

Wametoka kufungwa Jumatatu tu na Tottenham Hotspur ikiwa ni kipigo cha pili mfululizo EPL na hakika mashabiki wa Manchester United kwa sasa wana majonzi makubwa na hawaelewi nini kinatokea.

Wakati wakiendelea kuumia kutokana na matokeo mabovu, mshambuliaji anayesumbua sana EPL na Ulaya kwa ujumla kwa sasa Sadio Mane ameibuka na kupigilia msumari mwingine kwa United.Mane ameeleza sababu ya kukataa kujiunga na Manchester United 2015, sababu ambayo kila mshabiki wa United aliyeisikia ameishia kusonya tu kwa hasira.”Sikuamini kwanza kama walikuwa wananitaka, niliongea nao na hata kocha wao wakati huo (Louis Van Gaal) tulizungumza lakini kwangu niliona haikuwa timu sahihi mimi kwenda” amesema Mane.

Badala yake Sadio Mane aliiona Liverpool kama timu sahihi kwake na ndio sababu hakusita kusema “ndio” pale walipomtaka na inaonekana kwa sasa anaamini alifanya uamuzi sahihi kwani tangu ajiunge nao kiwango kimepanda na Liva wanacheza vizuri kuliko United.Sadio Mane pia ameongelea kuhusu Champions League na kusema kwamba baada ya kulikosa kombe hilo mwaka jana, anaamini safari hii tena wana uwezo wa kwenda fainali.

Kwa sasa Mane ni moja ya vinara wa mabao EPL akiwa na idadi sawa ya magoli pamoja na Lucas Moura, Sergio Aguero, Richarlison na Aleksander Mitrovic.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here