Home Kimataifa Wanampokea Pulisic lakini Hazard atabaki msimu ujao?

Wanampokea Pulisic lakini Hazard atabaki msimu ujao?

6828
0

Chelsea wamekamilisha usajili wa winga Christian Pulisic kutoka Borussia Dortmund kwa pauni milion 64. Pulisic anawasaidia kwanza Dormund kuwania ubingwa wa Bundesliga na ubingwa wa Uefa Champions League, halafu msimu ujao aanze mikimiki ya Ligi Kuu Uingereza.Chelsea wameamua kumaliza mapema, hawataki usumbufu kwenye majira yajayo ya kiangazi. Lakini moja ya swali kubwa ni kwamba, Hazard anabaki msimu ujao? Ingekuwa kombinesheni nzuri kuona Pulisic akitokea kulia na Hazard akitokea kushoto.Hazard amekuwa muhimu sana kwa Chelsea kwenye kutengeneza nafasi, kufunga, na kuamua matokeo.


Pedro (31, mkataba unaisha 2020)Willian (30, mkataba unaisha 2020)Hazard (27, mkataba unaisha 2020)


Msimu huu, Chelsea wamewategemea sana Hazard na Ngolo Kante katika kutengeneza nafasi za kufunga. Bila Hazard kuna tatizo kwa Chelsea. Itakuwa nafuu zaidi wakimbakisha Eden Hazard msimu ujao kuliko akiondoka.


Orodha ya sajili za gharama katika historia ya klabu ya ChelseaKepa Arrizabalaga (£71.6m)Álvaro Morata (£70m)Christian Pulisic (£57.6m)Jorginho (£57m)Fernando Torres (£50m)(Chanzo: Sky Sports)


Ukiona ujio wa Pulisic, tambua Willian au Pedro, kuna mmoja atatafuta mlango wa kutokea. Ni rahisi kukubali Willian aondoke lakini sio Hazard. Tatizo la Chelsea sio kwenye idara ya winga wa kulia ambalo wanacheza Willian na Pedro, ila hata kwenye idara ya ushambuliaji ni tatizo kubwa sana tangu Diego Costa ende zake Hispania.Kuna mechi niliona Maurizio Sarri akimpanga Hazard eneo analocheza Alvaro Morata. Hii ni kwasababu haridhishwi na idara ile ambayo wapo Morata na Giroud. Kumpanga Hazard namba tisa ni sawa na kumchezesha Ngolo namba saba.


Roberto Martinez- “Hazard ni mchezaji anayejali sana wachezaji wenzake sana. Ana roho ya kiupekee sijui kama akienda sehemu nyingine ataweza kuishi vizuri kama anavyoishi na wenzake Chelsea. Chelsea wanampenda sana. Mfumo wa Sarri na uwezo wake umeiviana sana. Hapaswi kuondoka” Hazard akicheza winga wa kushoto, Chelsea inakuwa bora zaidi maana nafasi nyingi za kufunga zinapatikana na timu inaonekana bora zaidi.Wakati Sarri anaendelea kuongeza ubunifu ndani ya uwanja na kutafuta mshambuliaji ambaye hawaangushi walioko nyuma yake, basi aombe Hazard abaki. Najua Hazard anaweza kuondoka na maisha yakaendelea lakini lazima upate shida kupata mbadala. Pulisic bado kijana mdogo aliyezaliwa mwaka 1998. Ana miaka 20 bado, hakuna anayewaza kwamba anakuja kuwa mbadala wa Hazard.Kila mtu anafikiria namna muunganiko utakavyokuwa endapo Pulisic na Hazard wakishirikiana kupika magoli pamoja na kufunga.Makala na Patrick Admila


Kidokezo: Kane amebakiza goli moja tu kuvunja rekodi ya Dwight Yorke ya mabao EPLHary Kane (Mechi 174 – Magoli 122)Dwight Yorke (Mechi 375 – Magoli 123)Yorke amecheza mechi 201 zaidi ya Hary KaneKane vs Mafowadi wengineKane 122 ⚽️ Mechi 174Yorke 123 ⚽️ Mechi 375Anelka 125 ⚽️ Mechi 364Keane 126 ⚽️ Mechi 349Hasselbaink 127 ⚽️ Mechi 288


Wachezaji bora wa BVB waliouzwa kwa gharama kubwa ndani ya miaka 3:📅 16/17:❌ Mkhi, Hummels, Gundogan, Blaszczykowski.💰 €111m.📅 17/18:❌ Dembele, Aubameyang, Ginter, Mor, Bender, Ramos.💰 €251m.📅 18/19:❌ Pulisic, Sokratis, Yarmolenko, Merino, Castro.💰 €114m.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here