Home Kimataifa “Wanaomtaka Rabiot wanapoteza Muda” Tuchel

“Wanaomtaka Rabiot wanapoteza Muda” Tuchel

8132
0
Thomas Tuchel amepuuza taarifa kuwa kiungo wake Adrien Rabiot ataondoka PSG, na kuwaomba mashabiki wa PSG kuwa na amani.


Rabioti ni mchezaji ambaye kwa sasa anasakwa na vilabu zaidi ya 6 na vyote vikiwa na nia ya dhati kabisa kunasa kalamu ya kiungo huyo.

Kwani taarifa zinasemaje?


Taarifa zilisema kuwa Barcelona wapo mbioni kumnasa kiungo huko. Lakini Tuchel amewakata maini vigogo hao wa  Camp Nou, kwa kusema Rabiot ni mali ya PSG na ataendelea kubakia klabuni hapo?Je kuna wengine wanammendea?

Hata hivyo vilabu vya Juventus, Bayern Munich na Chelsea vinafahamu fika kuwa Rabiot hana furaha sana klabuni hapo na anataka kuondoka. Inasemekana kuwa klabu ya Man City pia walifikia makubaliano na mchezaji hiyo ingawa taarifa hizo hazijathibitshwa na upande wowote. Fununu nyingine kutoka Liverpool na Tottenham zinasema kuwa kiungo huyo anahitajika kwa udi na uvumba Anfield na Hwite Hart Lane msimu ujao.


Lakini kocha wa PSG  Tuchel ameweka wazi kuwa hana mpango wa kumuuza  kiungo huyo wa France. Rabiot ni mmoja kati ya wachezaji wazuri waliochwa na Les Bleus kwemye kikosi kilichotwaa ubingwa wa dunia kule nchini Urusi.

                                  Taarifa binafsi
Majina Adrien Rabiot
Kuz 3 April 1995 (23)
Mah Kuz Saint-Maurice, France
Kimo 1.88 m (6 ft 2 in)
Naf KiungoTuchel anasemaje?

“Napenda kufanya kazi na Rabiot,” Tuchel alikiambia chombo cha RMC.

“Nampenda sana Adrien, najua alikumbwa sana na wakati mgumu kwa kutemwa kikosi cha tomy ya taifa, lakini ni chezaji wa muhimunsana kwenye kikosi changu”Vipi kuhusu nidhamu ya Rabiot?

“Hajawahi kunisumbua kwenye mazoezi na ni mchezaji ambaye hakosi mazoezini hata siku moja. Anajituma na ana moyo wa kufanya nami kazi”Kipaji na uwezo wake kwa ujumla?

“Ni mchezaji anayeweza kucheza aina yeyote ya mfumo na katika timu yeyote duniani, anaweza kucheza kwa kutumia nguvu na akili pia” Tuchel

Msimu Timu M G
2012–2014 Paris Saint-Germain B 9 (0)
2012–2018 Paris Saint-Germain 137 (12)
2013 → Toulouse (loan) 13 (1)

 

“Ana kipaji cha pekee, ni moja ya lulu kubwa za hapo baadae, ni jambo la kujivunia kuwa na mchezaji wa kariba hii”Amefanikiwa kutwaa mataji 16 na PSG.


Paris Saint-Germain
  • Ligue 1: 2013–14, 2014–15, 2015–16, 2017–18
  • Coupe de France: 2014–15, 2015–16, 2016–17, 2017–18
  • Coupe de la Ligue: 2013–14, 2014–15, 2015–16, 2016–17, 2017–18
  • Trophée des Champions: 2015, 2016, 2017, 2018

    Na Privaldinho

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here