Home Kimataifa Wanasemaje mkutano mkuu TFF Arusha?

Wanasemaje mkutano mkuu TFF Arusha?

3679
0

Maeneo yaliyofanyiwa kazi ni yafuatayo

1. Tumefanya mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 yaliyofanyika Dodoma kwa mtindo wa ligi

2. Tumeboresha programu za vijana na kuendesha katika mashindano mbalimbali

Rais TFF Wallace Karia


“Tutaanzisha Ligi ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 lakini pia tutaanzisha Ligi ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15,”- Rais TFF Wallace Karia


“Changamoto ambazo tunaziona zinazoonekana zitaathiri ligi Daraja la Kwanza tumeziona na tutazifanyia kazi,”- Rais TFF Wallace Karia


Mafanikio ya Soka la Ufukweni Tanzania kwenye viwango vya Ubora duniani tumepanda hadi nafasi ya 58 na kwa upande wa Afrika tupo nafasi ya 8 kwa hiyo tunaamini tunaweza kuingia hata kwenye 10 bora kwa Dunia,”- Rais TFF Wallace KariaRais Karia amesema kama kuna mtu anaungana na mtu aliyeiba pesa za TFF naye atashughulikiwa na kuongeza

“Kama kuna mtu anampenda aliyeiba fedha za TFF basi akae naye nyumbani kwake ampikie pilau”.


Uchaguzi mlishafanya na tunajua safu ya uongozi ilishakamilika lakini bado kuna watu wanataka kuirudisha TFF ilikotoka. Ombi langu kwenu ni msikubali :-Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo


Serikali ya Mkoa wa Arusha Tumetenga hekari 15 kwaajili ya kujenga uwanja wa kisasa wa michezo na TFF ndio watakaousimamia bila kupata usumbufu :-Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo


Mheshimwa Gambo umeutendea haki mpira. Hilo wazo la kujenga uwanja ni wazo zuri sana. Nawaomba wakuu wa mikoa wengine waige wazo hilo la kujenga uwanja- Rais wa heshima wa TFF, Leodger Tenga.


Mheshimiwa Rais wa TFF naomba niwapongeze kwa kazi mzuri mliyofanya na naomba muyaendeleze hayo mliyoyapanga, Leo tumesikia utekelezaji wa mipango hiyo na tunawapongeza sana :-Rais wa heshima wa TFF,Leodger Tenga.

#Mheshimiwa Rais wa TFF naomba niwapongeze kwa kazi mzuri mliyofanya na naomba muyaendeleze hayo mliyoyapanga, Leo tumesikia utekelezaji wa mipango hiyo na tunawapongeza sana :-Rais wa heshima wa TFF,Leodger Tenga.

#MkutanoMkuuTFFArusha2019

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here