Home Kimataifa Watanzania tuweke akiba ya maneno, tusiibeze Stars, na tusiwachukulie poa Cape Verde

Watanzania tuweke akiba ya maneno, tusiibeze Stars, na tusiwachukulie poa Cape Verde

10439
0

Uganda sio timu nzuri sana sawa nakubali na sio mbaya sana. Uganda hawana rekodi nzuri sana hivi karibuni, pia nakubali. Lakini Uganda wana wachezaji wengi wazoefu kutuzidi sisi. Uganda wao walikuwa na faida mara mbili. Kwanza wanachezaji takriban 9 wanaotoka ulaya, wana wachezaji 16 wanaocheza nje ya taifa lao. Kikosi chao cha mchezo wa mwisho ni wachezaji wawili tu waliotoka ligi yao ya ndani walifanikiwa kucheza.

Takwimu za mwisho za Uganda

08.09.18 ACN Uganda Tanzania 0 : 0  
02.06.18 RF Niger Uganda 2 : 1  
30.05.18 RF C.Africa Uganda 1 : 0  
27.03.18 RF Uganda Malawi 0 : 0  
24.03.18 RF Uganda S. Tome 3 : 1  
22.01.18 ANC Uganda I. Coast 0 : 0  
18.01.18 ANC Uganda  Namibia 0 : 1  
14.01.18 ANC Zambia Uganda 3 : 1  
17.12.2017 CHA Burundi Uganda  1 : 2  
15.12.2017 CHA Uganda  Zanzibar  1 : 2  

Kwa macho ya haraka haraka utagundua sio kwamba eti Uganda wana matokeo mazuri sana kuzidi sisi na Uganda ni pwagu na pwaguzi tu. Lakini hatuwezi kukataa kwamba wenzetu kidogo wamepiga hatua ukilinganisha na sisi. Uchezaji wao na wetu ni ule ule hii ndio sababu ya kusema hatuko mbali nao sana.Kiwango chao kimeimarika kwa kiasi fulani hasa ukiwalinganisha na sisi. Mwaka jana Walifuzu mataifa ya Afrika, lakini walifanya vibaya kwenye hatua ya makundi kwa kuambulia alama  moja tu.

T P W D L GF GA GD Pts
1  Zambia 3 2 1 0 6 2 +4 7
2  Namibia 3 2 1 0 3 1 +2 7
3  Uganda 3 0 1 2 1 4 −3 1
4 IvoryCoast 3 0 1 2 0 3 −3 1

Sioni sababu ya kuwaogopa sana Waganda. Tumewapa nafasi kubwa sana kisa tu wana Okwi anayetusumbua sana hapa ligi kuu. Hata hao wachezaji wao wa Ulaya wapo kwenye ligi za promosheni tu sio kwamba ni mastaa sana kiasi cha kutujaza vijasho kwapani. Sawa, kucheza nje kuna faida yake lakini wale bado saizi yetu tu. Tunasahau kwamba wao hawana mchezaji bora kama Mbwana Samatta. Hao Uganda wanaweza kuja hapa bongo na wakafa hata 3. Mchezo tuliopata nao Suluhu walikuwa uwanja wao wa nyumbani, walikuwa na mashabiki wote. Bado uwanja ulijaa maji na wanaujua zaidi uwanja wao na bado wakatepeta.

Wao walipaswa kulalamika zaidi kupata matokeo mabaya nyumbani kuliko sisi. Kocha wetu sie bado ni mpya naamanisha Amunike. Hajakaa kambini hata mwezi na timu ya taifa. Baadhi ya wachezaji yeye anawachagua aidha kwa sababu ameambiwa ni wazuri au wanacheza vilabu vikubwa na ni wachache sana tunaweza kukubaliana kwamba amewaona. Hivyo tuna kila sababu ya kuhifadhi baadhi ya maneno. Uganda wao kocha Sébastien Desabre yupo nao tokea  28 Decemba 2017, alipochukua nafasi ya Milutin Sredojevic(‘Micho’).

Kuhusu sakata la wachezaji kuachwa kawaida sana hiyo kwenye soka. Hatuwezi kukaa chini tujadili kwanini fulani kaachwa. Mwalimu alikuwa na muda mchache sana kukutana na wachezaji wake hasa ukizingatia wengi hawajui na hafahamu chochote kuhusu wachezaji hao. Sasa katika muda ule ule mchache bado mchezaji anajivuta (kama konokono, samahani) kana kwamba yeye ni bora kama akina Messi, kwamba wanapaswa wakaombwe jamani eeh kocha amesema njooni.

Tunajua kila mchezaji alikuwa na sababu zake lakini walipaswa kutoa taarifa mapema ili mwalimu ajue cha kufanya.

Kuna wengine wanalalamika kiwango cha Ulimwengu kibaya, Samatta kazingua n.k Hakuna mchezaji ambaye yupo fiti kwa mwaka mzima. Tena hasa kwa mazingira ya timu ya taifa ambapo wachezaji wengi wanakuja na falsafa tofauti tofauti, mbaya zaidi wapo wa Ulaya na hawa wenzetu wa changanyikeni.

Ni suala la muda tu. Bao alilokosa Samatta kawaida sana hiyo kwenye soka.


Kuna wakati mambo hayakai, kila unachokifanya kinakataa, ipo hivyo kwenye soka, sio kila siku utafanikiwa, mara kadhaa inatokea kila kitu hakiendi”  Abdi Banda.


Ndio mpira upo hivo. Kama uligundua Samatta alicheza zaidi jukumu la katikati ya uwanja. Na ukiangalia kwa necha ya uwanja ule ulivyokuwa mbovu n.k ilikuwa ni kazi sana kwa Samatta kwenda na kasi yake kwa kila kitu.

Samatta kweli ni kama tachi yake yampira akielekea kwenye penati boksi kama tageti yake ilikataa hivi mpira ukakimbia kwa kasi zaidi. Hiyo ni kawaida sana kama mpira una maji au uwanja pichi yake hajakaa sawa.

Samatta alichojaribu ni kwenda na kasi ya mpira ule lakini Onyango akatumia upenyo ule ule na kulijua wazo la Samatta. Chenga ya pili ilikuwa sahihi kwa Samatta maana kila engo alikabwa na mabeki wale. Lengo lake aidha kumpiga kipa chenga kisha atenge kwa mwenzake au afunge.


“Dhamira ya kila mchezaji wa Taifa Stars ni kucheza vyema, ili kusaidia timu kufanikisha malengo. Hakuna mchezaji anayekwenda kwa lengo la kuzingua” Privaldinho

Tugange yajayo.

Tunamchezo wa muhimu zaidi mbele dhidi ya Cape Verde. Stars itasafiri umbali wa kilometa 6875 mpaka mjini Praia kuwafuata Tubarões Azuis (Blue Sharks) au Crioulos (Creoles) hilo ndilo jina lao maarufu yaani Papa wa buluu.


Kuna watu wanadhani kuwa Cape Verde ni taifa dhaifu kisoka. Naomba niwaambie sisi hatujawahi kufika nafasi ambayo Cape Verde waliopo kwa sasa kwenye viwango vya FIFA.

Mchezaji wa Cape Verde akipewa kadi nyekundu kwenye mchezo wao dhidi ya Lesotho. Mchezo uliisha kwa 1-1

H2H ya Stars Vs Cape Verde

Tumekutana nao mara 3, Stars tukishinda mara moja (3-1) mwaka 2008 kwenye kufuzu kombe la dunia, na Cape Verde wameshinda mara moja (1-0) kule mjini Praia, na mchezo wa mwisho ulikwenda sare ya 1-1.

 Viwango vya Cape Verde
Ranki ya FIFA
Kwa sasa 64  (16 Aug 2018)
Viwango vikubwa zaidi 27 (Feb 2014)
Viwango vya chini 182 (April 2000)

Ukiangalia vizuri hao jamaa waliwahi kufika mpaka nafasi ya 27 duniani mwaka. Sisi nafasi yetu kubwa kabisa kuwahi kutokea ni nafasi ya 65.

Viwango vya Stars

Ranki za FIFA
Kwa sasa 140
(16 Aug 2018)
Viwango vikubwa 65 (Feb 1995)
Viwango vidogo 175 (Oct–Nov 2005)

Yaani Tanzania tulijikwamua weee mwaka 1979 tukafika karibia na nafasi ambayo Cape Verde waliopo kwa sasa. Cape sio taifa la kubeza hata kidogo. Cape Verde kwa sasa ipo juu kwemye viwango vya FIFa kuzidi magaifa makubwa na makongwe kwenye soka kama Misri, Ivory Coast na Guinea.

No Taifa alama
63 MLIMali 1360(1360)
64 CPVCape Verde Islands 1356(1356)
65 EGYEgypt 1355(1355.24)
66 ALGAlgeria 1351(1350.56)
67 CIVCôte d’Ivoire 1344(1344)
67 GUIGuinea 1344(1344)

Haijalishi taifa hilo halina wachezani maarufu kiasi gani lakini bado tunapaswa kujifunza kupitia namba zao ili tujue umakini wao uko wapi. Licha ya kwamba ni timu nzuri lakini bado ukiangalia ni timu dhaifu pia.

Takwimu za mwisho za Cape Verde.

05/09/17 WQA South Africa 1*2 Cape Verde
07/10/17 WQA Cape Verde 0*2 Senegal
14/11/17 WQA Burkina Faso 4*0 Cape Verde
02/06/18 FRI Algeria 2*3 Cape Verde
03/06/18 FRI Andorra 0*0 Cape Verde
09/09/18 ACO Lesotho 1*1 Cape Verde

Wakati sisi tukiburuzwa na Walgeria wa waliwapiga nyumbani kwao tatu. Waliwahi pia kuwafunga Afrika Kusini nyumbani kwao. Sio timu ya kubeza hata kidogo.

Kikubwa tunapaswa tujue Cape Verde asilimia 90 wachezaji wao wanacheza ulaya.

Naf Umri M G TM
GK Vozinha  32 24 0 Cyprus AEL Limassol
GK Iván Cruz 22 0 0 Portugal Gil Vicente
GK Thierry Graça  23 0 0 Portugal Estoril

DF Fernando  30 41 3 Greece PAOK
DF Gegé  30 25 2 Saudi Arabia Al- Fayha
DF Carlitos  33 23 0 Portugal Real SC
DF Tiago Almeida 27 3 0 Portugal Uniao Madeira

MF Babanco 33 44 3 PortugalFeirense
MF Marco Soares 34 32 0 Portugal CD Feirense
MF Nuno Rocha 26 10 0 Russia Tosno
MF Manú 30 5 0 PortugalLeixões
MF Jamiro Monteiro 24 4 0 NetherlandsHeracles Almelo
MF Carlos Ponck 23 1 0 Portugal Aves
MF Hélder Tavares 28 1 0 PortugalTondela

FW Wuilito Fernandes 28 3 0 United States North Carolina FC
FW Júlio Tavares 29 15 2 France Dijon
FW Ze Luis 27 14 2 RussiaSpartak Moscow
FW Garry Rodrigues 27 18 2 TurkeyGalatasaray
FW Kuca 29 14 1 PortugalBoavista
FW Jovane Cabral 20 1 0 PortugalSporting CP B

Wana mchezaji wa Galatasaray, yupo wa Dijon ya Ufaransa, yupo wa Spartak Moscow na wengi wanacheza Ureno kutokana na taifa hilo kutawaliwa na Ureno kwa kipindi kirefu.


Kilichobaki ni Amunike kutumia mbinu zote alizopata akiwa Barcelona kuhakikisha angalau tunapata alama moja au 3 kule ugenini kuliko tufungwe kisha wakija hapa tuhakikishe uwanja mzima unajaa na kuwatia moyo vijana tuibuke na alama 3.

Mashabiki wa Uganda walijaa uwanja mzima na wote walivalia jezi za timu yao na walishangalia kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya 95

Licha ya kwamba ni wazuri lakini wakati fulani mpira sio majini. Mchezo wao wa kwanza katika kundi hili walifungwa nyumbani bao 1 na Uganda mchezo wao wa pili wametoka sare na Lesotho Ugenini.

Hatuwezi kuwadharau Lesotho kwa sababu hao hao walipata sare ya 1-1 hapa hapa uwanja wetu wa taifa. Kundi letu ni rahisi sana kama tukijipanga vyema. Alama 3 kule Lesotho inawezekana kabisa, hapo tutakuwa tumefikisha alama 5, alama 3 au 1 ugenini kule Cape Verde tutakuwa na alama 8 au 6. Hata kama uganda atashinda michezo miwili ya Cape Verde nyumbani na Lesotho zote atakuwa na alama 12 ataongoza kundi, lakini sisi akija hapa tumbutue tufikishe alama 12 au 9. Kimahesabu tutshika nafasi ya pili. Ni kujitambua tu na kucheza kitimu zaidi kuliko kucheza kiujuaji.

Asilimia 99.0 wachezaji wa stars hatuchezi kwa falsafa ila tunacheza kwa jitihada. Samatta pekee ndiye mchezaji tunayesema anacheza soka la Falsafa kwa kuwa mara nyingi Ulaya mpira wao ni wa falsafa lakini mpira wa huku changanyikeni mchezaji amacheza kwa jitihada zake na kijituma ili kumfurahisha mwalimu na mshabiki.


Naitwa Privaldinho unaweza pia kunifollow Instagram, usiache kufollow pia page zote za shaffih dauda facebook na Instagra. Pia tupo youtube kupitia Channel ya Dauda Tv

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here