Home Kitaifa Wawa katoboa siri Simba

Wawa katoboa siri Simba

13779
0

Na Tima Sikilo

BEKI wa Simba Pascal Wawa, amesema siri ya kuongezeka kwa kiwango chake ni mazoezi anayoyafanya kila siku bila kujali changamoto anazo kutana nazo.

Wawa amesajiliwa na Simba katika dirisha kubwa la usajili msimu huu akitokea nchini kwao Ivory Coast akiwa mchezaji huru.

Amesema amefurahia timu yao kupata ushindi katika mchezo wa kwanza waligi huku akiwa ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi hicho cha ushindi.

Wawa ameongeza kuwa anamshukuru Mungu kwa kuongezeka kwa kiwango chake cha uchezaji tofauti na ilivyokuwa mwanzo na hiyo nikutokana na kuzingatia mazoezi anayoyafanya.

“Nafurahi kuona timu yangu imepata ushindi katika mchezo wa kwanza wa ligi nikiwa miongoni mwa kikosi hicho kwa mara ya kwanza, kiwango changu ni tofauti na nilivyokuja kutokana na juhudi katika mazoezi naamini nitazidi kuwa bora siku za mbele, “amesema Pascal Wawa

Simba jana walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Taifa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here