Home Kimataifa Weah “Ukiacha Mungu, Wenger alifanya nifanikiwe kwenye soka”

Weah “Ukiacha Mungu, Wenger alifanya nifanikiwe kwenye soka”

12884
0

Arsene Wenger amepewa tuzo ya heshima kutoka kwa Raisi George Weah.

Ukijaribu kuangalia tukio hili linatoa tafakari ya kipekee. Unajiuliza kwanini Weah amemchagua Wenger. Kuna kitu kipo katikati ya hawa jamaa wawili ambao pia waliwahi kufanya kazi.

Wenger alimsainisha Weah mwaka 1988 alipokuwa akiitumikia Monaco miaka 7 iliyofuata Weah aliweka historia ya kuwa muafrika pekee kutwaa tuzo ya Ballon d’Or.

ARSENE WENGER

“nilikuwa na rafiki yangu ambaye alikuwa akifanya kazi Afrika akawa anamuulizia kuhusu uwezekano wa kupata mshanbuliaji mzuri. Yule rafiki yake moja kwa moja akamwelekeza kwa Weah. Nikaongea nae akakubali kujiunga nasi kwa dau la £50,000.

Alikuwa mchezaji wa kipekee. Alijituma alikuwa na akili na uwezo mkhbwa sana uwanjani. Hata wakati anabeba tuzo ya mchezaji bora duniani hakuna ambaye alipatawa shaka. Capello, Lippi wote walikuwepo lakini wakimvukia kofia”

Raisi Weah amemkaribisha Wenger nchini Liberia. Wenger ni mtu wa kawaida tu kama watu wengine lakini ameitwa kwa heshima na raisi wa nchi. Sio kwamba Wenger ni bilionea labda ameitwa kuwekeza. Hapana. Ameitwa kwa heshima kabisa ili kupewa tuzo ya heshima.

Ni jambo la kipekee. Weah anatuonesha kuwa kufanikiwa sio kujitenga ila ni kulipa fadhila. Walio wengi tukifanikiwa huwa tunapuuzia tulikopita.

Weah anayuonesha kuwa Wenger ana mengi ya kukumbukwa na dunia ya Afrika kwa ujumla.

Ameinua vipaji vya wachezaji wengi wa Afrika. Yeye ni tofauti kabisa na wale makocha wanaosubiria mchezaji awe bora ndipo amtwae. Wenger alimchukua Weah akiwa hajulikana popote zaidi ya Cameroon na Liberia. Hakuwa na jina kubwa kisoka. Lakini nani alijua kuwa mwaka 1995 kama Weha angekuwa mchezajibbora duniani?

Pia wakati Wenger anamnunua Weah hakuwahi kufikiria kwamba ipo siku Weah atakuwa Raisi wa nchi. Leo hii Weah amekuwa raisi na amelipa fadhila kwa kumtunuku “Knight Grand Commander of the Humane Order of African” kwa kulipigania soka la Afrika.

Katika kipindi cha miaka 30 Wenger ameinua vipaji vya waafrika wengi sana wakiwepo Nwankwo Kanu, Lauren, Kolo Toure na Emmanuel Adebayor.

ORODHA YA WACHEZAJI WA KIAFRIKA CHINI YA WENGER

Emmanuel Adebayor (Togo), Alex Iwobi (Nigeria), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon), Nwankwo Kanu (Nigeria), Marouane Chamakh (Morocco), Lauren (Cameroon), Kaba Diawara (Guinea), Quincy (Ghana), Emmanuel Eboue (Ivory Coast), Alex Song (Cameroon), Mohamed Elneny (Egypt), Kolo Toure (Ivory Coast),
Emmanuel Frimpong (Ghana), Armand Traore (Senegal), Gervinho (Ivory Coast) and Christopher Wreh (Liberia).

Mandela aliwahi kumsihi George Weah anapaswa kulikumbuka taifa lake. Asisahau kuwa anajukumu la kupigania taifa lake. Nadhani Weah amelitumia somo la Mandela vyema na hajakumbuka taifa pekee yake amemkumbuka na Arsene Wenger.

“Nilipowasili Monte Carlo nilikuwa nimetokea klabu ya Tonnerre Yaoundé mwaka 1988. Sikufanikiwa kucheza miezi 6 ya mwanzo. Arsène Wenger alikuwa kocha wangu. Alinilea kama mtoto mdogo. Nilikuwa nabaguliwa sana. Sikuwa na amani hata kidogo. Siku mojaa wakati wa mazoezi nilikuwa nimechoka sana. Nikamfuata mwalimu [Wenger] nikamweleza kichwa kinauma.

Akaniambia (Najua ni kazi sana, najua mazoezi ni magumu sana lakini kutokana na kipaji chako unapaswa ujitume kwa kiwango cha hali ya juu sana) Sitaki kuwa muongo. Nilifurahi sana. Nilirudi nikaendelea na mazoezi. Sikuwa nimechoka kweli ika tu ni hasira na uvivu kwa namna niliyokuwa nikinyanyaswa na watu wengine.

Kusema kweli ukitoa Mungu, mtu aliyenifanya nifanikiwe ulaya ni Arsenal Wenger”

MAFANIKIO YAKE

1995 Paris Saint-Germain
1995 Paris Saint-Germain
1995 Paris Saint-Germain
1994 Paris Saint-Germain
1989 AS Monaco
98/99 Serie A
95/96 Serie A
2000 FA Cup
94/95 UEFA Champions League
2002 Liberia
1996 Liberia
93/94 Ligue 1
94/95 Coupe de France
92/93 Coupe de France
90/91 Coupe de France
94/95 Coupe de la Ligue

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here